Mafunzo ya Ujasiriamali

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anawatangazia wahitimu wote wa elimu ya juu kuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimeandaa mafunzo ya ujasiriamali yatakayotolewa katika mikoa kumi na moja ya Tanzania (Tanzania Bara na Zanzibar) mwezi Oktoba na Novemba mwaka 2021. Mafunzo haya yanatolewa kama sehemu ya huduma kwa jamii inayofanywa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.